Neno la leo limetoka katika kitabu cha Mithali 16:1-9
1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.
2 Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu.
3 Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.
4 Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.
6 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.
7 Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.
8 Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.
Waliotungozea neno la leo ni Selina Mdimi (Mama Rhoda), Clara Gama na Emmanuel Sebastia.
Saturday, March 7, 2015
Saturday, February 28, 2015
JUMAMOSI YA NENO
Neno la leo limetoka katika kitabu cha Nabii Yeremia 33:1-6
1 Tena, neno la Bwana likamjia Yeremia mara ya pili, hapo alipokuwa akali amefungwa katika uwanda wa walinzi, kusema,
2 Bwana alitendaye jambo hili, Bwana aliumbaye ili alithibitishe; Bwana ndilo jina lake; asema hivi,
3 Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
4 Maana Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;
5 Wanakuja kupigana na Wakaldayo, lakini ni kuzijaza kwa mizoga ya watu, niliowaua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, ambao kwa ajili ya uovu wao wote nimeuficha mji huu uso wangu.
6 Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.
Waliotungozea neno la leo ni Mwlm Peter Mzuli, Innocent Mosha na Marystella Leonard

Thursday, February 26, 2015
MUNGU ASANTE
Tuna kila sababu ya kusema Mungu asante kwa kila hatua tunayoipitia, tunaamini kuwa kupitia maombezi ya Mtakatifu Lucia, tutasimama imara katika kumteteaYesu Kristu aliye njia ya kweli na uzima. Na pia kulitangaza neno la Mungu kwa njia ya uimbaji. Tunaziombea kwaya zote ziweze kuinjilisha katika Roho na Kweli. Amina
Haya ni mahudhurio ya kawaida kwa sauti ya kwanza
Hawa ni baadhi ya sauti ya Pili
Hawa ni baadhi ya Sauti ya Tatu
Na hawa ndio baadhi ya wababa wa kwaya(yaani sauti ya nne)
Saturday, February 21, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)