Saturday, March 7, 2015

JUMAMOSI YA NENO

Neno la leo limetoka katika kitabu cha Mithali 16:1-9
1  Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.
2  Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu.
3  Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.
4  Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
5  Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.
6  Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.
7  Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.
8  Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9  Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.


Waliotungozea neno la leo ni Selina Mdimi (Mama Rhoda), Clara Gama na Emmanuel Sebastia.